kiswahili-ulimbwende.docx

June 11, 2018 | Author: Augustino Emmanuel | Category: Documents


Comments



Description

CHUO KIKUU CHA MTAKATIFU AGUSTINO TANZANIA
(Chuo kikuu kishiriki cha askofu mkuu Yakobo)
KITIVO CHA SANAA NA SAYANSI YA JAMII
IDARA YA LUGHA NA ISIMU
JINA LA KOZI : NADHARIA ZA UHAKIKI NA MAENDELEO YA
FASIHI YA KISWAHILI
MSIMBO WA KOZI : KF 122
JINA LA MHADHIRI : MWL. NGOLE
AINA YA KAZI : KAZI YA KUNDI
JINA LA KUNDI : FLAMINGO
MAJINA YA KIKUNDI
NA
JINA LA MWANAFUNZI
NAMBA YA USAJILI
SAHIHI
1
AHMADI REHEMA
BAEDI-2016/009

2
ALLY SADICK MSUA
BAEDI-2016/015

3
BENARD MUSA
BAEDI-2016/055

4
BUNDALA FILBET
BAED1 2016/066

5
BURA DAUDI Y
BAEDI-2016/069

6
CHISONGELA SIMON ADAM
BAEDI-2016/089

7
DARABE YUSUPH K.
BAEDI-2016/099

8
FELIX DENIS T.
BAEDI-2016/150

9
HANKUNGWE KRIAD
BAEDI-2016/179

10
IDDI ABASI YAHAYA
BAEDI-2016/196

11
LAURENT EMIL ALEX
BAEDI-2016/375

12
MMBAGA EDDBILY E.
BAEDI-2016/553

13
MUSHI JAQUELINE J.
BAEDI-2016/610

14
MWAKUNA HADIJA K.
BAEDI-2016/629

15
NDABITA MPAWE A.
BAEDI-2016/677

16
REDDY AIDA
BAEDI-2016/785

17
ROBERT ZAKAYO
BAED-2016/788

18
SIMON MHOJA
BAEDI-2016/862

19
MPANGALA EMMANUEL M.
BAEDI-2016/957

20
ZAMAN THOMAS MARTIN
BAEDI-2016/939

SWALI 19: Linganisha na ulinganue ulimbwende wa kimagharibi na wa waswahil
MPANGO KAZI
Mjadala wetu umegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni utangulizi, kiini na hitimisho. Katika utangulizi tumeangalia dhana ya ulimbwende katika hali ya kawaida pamoja na nadharia ya ulimbwende wa kimagharibi na ule wa waswahili, asili ya ulimbwende wa kimagharibi na ule wa waswahili, uromansia, waasisi wa dhana hizi mbili, maoni ya dhana hizi mbili katika fasihi, sifa pamoja na misingi ya ulimbwende katika kazi ya fasihi, jinsi tapo la ulimbwende linavyojitokeza katika kazi ya fasihi ya Kiswahili, pamoja na mafanikio na upungufu wa dhana hizi mbili za ulimbwende yaani ule wa kimagharibi na wa waswahili kwa kuwarejea wataalamu kama vile Wordworth William, na Coleridge Samwel, Mulokozi, K Kahigi, Shafi Adam Shafi, Muhamad S Khatibu, Penina Muhando, Euphrase Kezilahabi na Theobard Mvungi . Pia katika upande wa kiini tumeangalia kufanana na kutofautiana kwa ulimbwende wa kimagharibi na ule wa waswahili. Na kipengele cha mwisho tumehitimisha kwa kuonesha mawazo ya jumla kuhusu nadharia ya ulimbwende. Vile vile katika mjadala huu tumewarejea waasisi mbalimbali kama vile Wamitila, K.W (2003), Emmanuel Kant (1772-1804) na Mathew Anold (1822-1888).
MAANA YA ULIMBWENDE
Ulimbwende ni urembo, au uzuri uliopo katika kitu fulani, hususani yaweza kuwa katika mavazi, katika nywele na umbo.
Baada ya kuona maana ya ulimbwende ni vema tukaangalia nadharia ya ulimbwende kama ilivyojadiliwa na Wamitila (2003).

1
NADHARIA YA ULIMBWENDE
Wamitila (2003), Ulimbwende ni istilahi inayotumiwa kuelezea sifa za sanaa, mziki, falsafa na fasihi za Ulaya na Marekani mwishoni mwa karne ya 18 namwanzoni mwa karne ya 19.
ASILI YA NADHARIA YA ULIMBWENDE WA KIMAGHARIBI
Kuna mitazamo tofauti juu ya chimbuko la ulimbwende wa kimagharibi kwani wataalamu mbalimbali wanatoa mawazo yao juu ya asili na chimbuko la ulimbwende wa kimagharibi kama ifuatavyo:-
Wafula na Njogu (2007:55), wanadai kuwa, katika fasihi ya kimagharibi ulimbwende ulifuata urasmi mpya moja kwa moja. Wanazidi kusema kuwa ulimbwende wa kimagharibi umegawanyika katika aina kuu mbili, yaani ulimbwende uliojitokeza katika karne ya kumi na mbili na kumi na tatu na ule uliojitokeza katika karne ya kumi na tisa.
Ulimbwende wa kimagharibi katika karne ya kumi na mbili na kumi na tatu.
Huu ulikuwa na muelekeo wa kusimulia ambapo wahusika wake walikuwa mashujaa, wenye nguvu za ajabu na ambao walikuwa wanajeshi. Jambo linaloufananisha ulimbwende huu wa awali na ulimbwende wa baadaye (yaani wa karne ya 19) ni kwamba wasimulizi wa wahusika waliosawiriwa walikuwa huru kutenda mambo waliyotenda. Ulimbwende uliotokea karne ya kumi na tisa (19) ulikuwa na mwelekeo wa kinadharia na upinzani dhidi ya urasmi mpya wa kimagharibi
Ulimbwende wa kimagharibi karne ya kumi na tisa (19)
Ulimbwende huu ulikuwa wa kitaalanu uliochipukia mnamo karne ya 19 na ambao uliandamana na matumaini ya fanaka katika ngazi mbalimbali za maisha ya mwanadamu.
2
Ni mtazamo uliotia fora kati ya mwaka wa 1800 na 1850. Japokuwa mtazamo huu wa fasihi ulisambaa sehemu mbalimbali za Uropa katika miaka tofauti tofauti. Waingereza wawili walisababisha kuenea kwake kama mkabala wa kitaalamu wa kuishughulikia fasihi. Wataalamu hao walikuwa ni William Wordworth na Samuel T. Coleridge (Blamires, 1991).
Majira ya ulimbwende yalikuwa ya kimapinduzi katika mwaka wa 1789, mapinduzi ya kisiasa yalitokea huko Ufaransa. Sehemu zingine za Uropa (Europe) zilitetemeshwa na matokeo ya mapinduzi haya. Hali hii ilikuwa kinyume na muktadha uliopalilia, kukuza na kuimarisha urasmi mpya.
Ulimbwende asili yake ilitokea katika sehemu ya Medieval katika udhaifu wa Romance ya Ufaransa ukiwa na maana ya riwaya na baadaye uliingia Ujerumani na Uingereza.Ulitokea karne ya 18 na 19 baada ya mapinduzi ya viwanda, zilikuwa ni nyakati za kutumia akili na za mwamko.Tapo hili lilikua ni matokeo ya msisimko ambao ulikua ni wakifasihi, kifasalfa, kidini nasanaa. Hivyo ulimbwende uliambatana na mawazo ya kimaendeleo ya siasa za nyakati hizo, wanafalsafa na wanasayansi waliokua maarufu na walioathiri jamii wakati huo ni Emmanuel kant(1772-1804) kutoka Ujerumani aliibuka na ufafanuzi wa kibinafsia enzi nuru akilinganisha dhana ya "building" (yenye maana sawa na utamaduni). Pia mwingereza Mathew Anold (1822-1888) alitumia neno "Utamaduni" kumaanisha hali ya juu ya sanaa ya ubora wa binadamu ambao uliwai kuwaziwa na kusemewa ulimwenguni na pia aliona utamaduni kama fujo, walimbwende wengine huko uingereza waliona kama nyikani au hali ya kimaumbile, waliona utamaduni wa juu ulivyoharibu hali ya kimaumbile mfano ni Edward Taylor alieleza hivyo.
3
Baada ya kuangalia asili ya nadharia ya ulimbwende wa Magharibi kama ilivyo jadiliwa na wataalamu mbalimbali hapo juu. Nivyema tukaangalia Uromansia (Romance)/ ulimbwende kwa ufupi.
UROMANSIA (ROMANCE)/ULIMBWENDE
Kazi za kiromansia ni kazi ambazo haziakisi hali ya jamii. Ni kipindi ambacho kazi ya sanaa ilikuwa kwa ajili ya burudani tu. Ulizuka na kutamalaki huko ulaya kuliko huku Afrika, hasa wakati wa mapinduzi ya viwanda. Badala ya fasihi kuonya unyanyasaji wa wafanyakazi fasihi ilijishughulisha na kuburudisha jamii na kupongeza tabaka la juu ilisisitiza masuala ya mahaba na mapenzi ilisahau kabisa masuala ya kijamii.
Pia baada ya kuona au kuangalia uromansia kwa ufupi sasa tunaenda kuangalia ulimbwende wa kimagharibi za waasisi wake.
ULIMBWENDE WA KIMAGHARIBI NA WAASISI WAKE
Baadhi ya wataalamu mbalimbali walioongelea kuhusu ulimbwende wa kimagharibi ni pamoja na Wordworth William, na Coleridge Samwel ambao wanasema mwelekeo wa ulimbwende kinadharia ulikuwa ukileta ukinzani dhidi ya urasmi mpya wa kimagharibi. Athari za viwanda vilielekea kuenea kwa fasihi katika maeneo mengi huko ulaya kutokana na nadharia ya ulimbwende. William Wordworth alitetea demokrasia na uhuru wa mtu dhidi ya utumwa na dhuluma wa wanajamii wengi kupitia masuala aliyoyatunga.
Baada ya kuangalia ulimbwende wa kimagharibi na waasisi wake kwa ufupi ni vyema pia tukaona maoni ya walimbwende wa kimagharibi kuhusu fasihi.
4
MAONI YA WALIMBWENDE WA KIMAGHARIBI KUHUSU FASIHI
Juu ya chanzo cha fasihi, walimbwende hawa wanasema fasihi ni zao la mtu binafsi, hivyo wanasisitiza ubunifu wa msanii katika utunzi kwa sababu ni kazi yake. Hivyo basi mtunzi wa kazi ya fasihi yoyote ni lazima awe mbunifu kwa kutunga kazi za kifasihi zinazokubalika na wasomaji.
Pia waasisi waliafikiana kuwa msanii azingatie ubunifu unaomwezesha kutunga kazi nzuri. Hii ina maana kuwa mbunifu au msanii asifungwe na sheria bali afuate hisia zake jinsi zinavyomwongoza. Maoni yao juu ya fasihi ya ulimbwende wanasema ulimbwende ni ni uelekeo mpya wa msingi wa mtunzi wa kazi ya kifasihi na wanasema wameasi kufuata sharia za uhakiki na badala yake wanafuata hisia zao.
Maoni yao kuhusu maana ya ushairi. Kwao ushairi ni hisi zenye nguvu zinazobubujika bila kuteguliwa wala kuzinduliwa katika moyo wa mtunzi. Ni bubujiko la hisi nyingi zinazojisababisha zenyewe. Hisi hizo ndizo muhimu katika utungaji wa shairi. John Keats mmoja wapo wa walimbwende wa kiingereza wa wakati huo. Amenukuliwa akisema "kama ushairi hautoi na kutoka kinywani mwa ushairi kiasili mathalani matawi yanavyoota mtini, hapana haja ya kuwa na ushairi huo". Hivyo basi ushairi unapaswa kumsawiri binadamu katika hali yake halisi.
Pia walizungumzia kuhusu dhima ya ushairi. Wanasema kwamba ushairi unapaswa kusisimua na pia, unatarajiwa kuzindua hisi na moyo wa msomaji au mhariri. Karne ya kumi na nane na kumi tisa zilishuhudia matukio yaliyosababisha ukengeushi katika maisha ya watu. Baadhi ya matukio haya yalikuwa, mauaji yaliyotokana na mapinduzi,

5
maisha ya mjini, na kazi za viwandani zilizoleta pesa, utajiri na umaskini mwingi. Ushairi wa kilimbwende ulinuia kuwaafikisha walimwengu na ulimwengu wao uliokuwa katika vuguvugu la madiliko ya kasi.
Baada kuona maoni ya walimbwende wa kimaharibi kuhusu fasihi. Sasa ni vyema tukaangalia mafanikio ya ulimbwende wa kimagharibi kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007:58).
MAFANIKIO YA ULIMBWENDE WA KIMAGHARIBI
Ulimbwende ulikuwa karibu na hali halisi ya wanadamu kuliko urasmi mpya wa kimagharibi
Ulisawiri namna ya kuwaza na kuwasilisha fikra kwa urahisi.
Umuhimu wa hisi katika utungaji ulioneshwa.
Pia baada ya kuona mafanikio ni vyema sasa tukaangalia mapungufu ya ulimbwende wa kimagharibi kwa ufupi kwa mujibu wa Njogu na Wafula (2007:59).
UPUNGUFU WA ULIMBWENDE WA KIMAGHARIBI
Kule kusisitiza hisi kuliangusha ulimbwende wa kimagharibi. Hapo baadaye, hisi zilisisitizwa sana ikawa hazina umuhimu wala maana tena.
Ulimbwende ulianza kushughulikia mambo ya kidhahania ilhali matatizo ya watu yalikuwa ya kihalisia, jambo hili liliufanya ulimbwende kupitwa na wakati.
Nadharia ya ulimbwende wa kimagharibi ilizungumzia ushairi peke yake, haikuzingatia tanzu nyingine za fasihi.

6
Baada ya kuona upungufu wa ulimbwende wa kimagharibi ni vyema tukaangalia sifa za ulimbwende katika kazi ya fasihi.
SIFA ZA ULIMBWENDE KATIKA KAZI ZA FASIHI ZA KISWAHILI
Katika kazi za fasihi za Kiswahili kuna kazi baadhi zilitungwa kwa kufuata ulimbwende huu kwa sifa hizi zifuatazo;
Utumizi wa wahusika wa ajabu. Wahusika wa ajabu katika kazi ya fasihi walianza kujitokeza, wahusika hao ni kama vile Mazimwi, mashetani, machizi na walevi ambao walitumiwa katika kazi za fasihi tofauti na wanaurasmi, mfano CHOZI LA SAMIRA, MADONDA NDUGU, KIVULI KINAISHI na NGUZO MAMA
Uumbaji wa hali za kushangaza zinazoambatana na matukio ya kustaajabisha kama vile, miujiza na ndoto. Kazi nyingi za fasihi ziliandikwa kwa mitazamo ya ndoto ambazo zilitofautiana na kazi za wana Urasmi, mfano CHOZI LA SAMIRA, KUSADIKIKA, MADONDA NDUGU na THE GREAT POND.
Kuzingatia dhamira zinazotetea utu, mapenzi, uadilifu katika matendo ya binadam. Kazi nyingi za ulimbwende zilitungwa bila uadilifu wowote bali zilijikita katika kutetea masuala ya msingi ambayo yalijitokeza katika jamii. Mfano KIU YA HAKI, NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE na diwani ya MAPENZI BORA.
Kuibuka kwa fasihi ya majaribio. Kutokana na kuibuka kwa fasihi ya majaribio, kumekuwa na matumizi ya mfumo mpya ndani ya mfumo wa zamani kama vile, matumizi ya nyimbo, hadithi ndani ya masimulizi mfano, CHOZI LA SAMIRA, KIVULI KINAISHI, MADONDA NDUGU, MORANI na TAKADINI.
7
Pia baada ya kuangalia sifa za ulimbwende katika kazi ya fasihi ni vyema pia tukajadili misingi ya ulimbwende katika kazi ya fasihi.
MISINGI YA ULIMBWENDE KATIKA KAZI YA FASIHI
Wanaulimbwende walipinga sheria zilizowekwa na wanaurasmi mpya na mkongwe, kwa mfano wanaulimbwende walipinga matumizi ya lugha ya juu kwa ajili ya hadhira ya matajiri na ya chini kwa watu wa kawaida.Mgawanyo wa hadhira ulikiukwa na wanaulimbwende.
Walimbwende walisisitiza pia utetezi wa haki za binadamu, dhamira ambayo hapo awali katika tapo la urasmi halikuweza kushughulikiwa. Msingi huu katika uhakiki wa kazi ya fasihi umejitokeza katika kazi mbalimbali za fasihi.
Walimbwende pia walianza kuandika juu ya nyakati za utoto wao. Walianza kuunda wahusika wa ajabu ajabu katika kazi zao za fasihi wahusika ambao warasmi hawakuwathamini. Walimbwende walidiriki hata kuwafanya hawa wahusika wa ajabu ajabu kuwa ni wahusika wakuu wakazi zao za fasihi, hapa basi shetani,walevi, jangili, wavunja sheria na wengine wa aina hii walizuka kuwa wahusika muhimu wa kazi za fasihi za walimbwende.
HISTORIA YA NADHARIA YA ULIMBWENDE WA KISWAHILI
Kulingana na machapisho mbalimbali ya wataalamu wakiwemo Njogu na Wafula pamoja na Wamitila tunabaini kwamba historia ya ulimwengu wa fasihi ya Kiswahili, hakuna nadharia ya ulimbwende wa waswahili bali nadharia hii inajipambanua kutokana na kazi mbalimbali
8
zilizoandikwa na wasanii zikizingatia miongozo ya ulimbwende hasa baada ya mapinduzi ya
viwanda mwaka 1960 na kuendelea, yaani sifa za ulimbwende wa kimagharibi ikiwa ni pamoja na:-
Utumizi wa wahusika wa ajabu
Sifa za ushujaa, miongoni mwa wahusika hao zilizingatiwa.
Hali ya kushangaza kama vile miujiza hazikuwa nadra kutokea.
Maudhui ya mapenzi ndiyo yaliyozingatiwa zaidi.
Masimulizi aghalabu yalikuwa thibitisho la fundisho fulani. Njogu na Wamitila (2007:59)
Mifano ya kazi hizo ni pamoja na TAKADINI (Benhanson), MFADHILI, KUFIKIRIKA, CHOZI LA SAMIRA, pamoja na MADONDA NDUGU.
MISINGI YA ULIMBWENDE KATIKA FASIHI YA KISWAHILI
Miongoni mwa misingi ya ulimbwende katika fasihi ya Kiswahili ni pamoja na utumizi wa lugha rahisi nayakawaida inayoeleweka na hadhira yeyote. Ilipinga matumizi ya lugha ya juu ilikuepusha utabaka, mifano ya kazi hiyo ni Watoto wa mama ntilie, MFADHILI, USIKU UTAKAPOKWISHA, MBIVU YA MAMA, na KIU YA HAKI. Hivyo ndivyo walimbwende walivyo faidi matunda ya uhuru wa muandishi hasa baada ya kuzuia utabaka uliojitokeza katika kazi hizo.
Utetezi wa haki za binadamu pia ulikuwa ni msingi wa kazi za walimbwende ambapo hii ilikuwa ni dhamira iliyokosa kushughulikiwa hapo awali, msingi huu
9
umejitokeza katika kazi kama zifuatazo, MBIVU YA MAMA inayotetea uhuru wa mwanamke, MADONDA NDUGU katika utetezi dhidi ya tabaka kandamizi, NGUZO MAMA na VUTA NIKUVUTE. Hivyo walimbwende walikuwa na shabaha ya kumtetea binadamu katika nyanja zote kwani hapo awali haikuwa hivyo.
Pia walimbwende walianza kuandika juu ya nyakati za utoto wao pamoja na uundaji wa wahusika wa ajabu ajabu ambao hapo awali warasmi hawakuwathamini pia walidiriki kuwafanya wahusika wakuu mfano, Mashetani, walevi, jangili, wavunja sheria na wengine walizuka katika kazi za fasihi, mfano Maisha yangu na baada ya miaka hamsini. Shaaban Robert (1934-1945) Riwaya ya wasifu,
JINSI TAPO LA ULIMBWENDE LINAVYO JITOKEZA KATIKA KAZI YA FASIHI
YA KISWAHILI
Ulimwende katika fasihi ya Kiswahili unaonekana zaidi katika ushairi hasa katika mgogoro uliozuka baina ya wanajadi wa ushairi wa Kiswahili na wanausasa miaka ya 1960.Baadhi ya wanausasa walio kuwepo wakati huo ni Mulokozi, K. Kahigi, Shafi Adam Shafi, Mohamed S. Khatibu, Penina Muhando, Euphrase Kezilahabi na Teobard Mvungi, Hivyo ulimbwende ni mawazo ya kimapinduzi ya kisanaa ambayo yalilenga kuzikana sheria za urasmi mkongwe na ulimbwende mpya ambapo msanii hakuwa na uhuru katika kazi yake. Hivyo nadharia ya ulimbwende iliweza kujibainisha kwa misingi mbalimbali ambayo nitofauti na urasmi mkongwe na urasmi mpya, Tapo la ulimbwende limejitokeza katika fasihi ya kiwahili kama ifuatavyo;
10
Waandishi watapo hili walipinga mgawanyo wa mada ambao ulikataa kuongea kuhusu watu wa kawaida.Walimbwende sasa walianza kuongea kuhusu wachuuzi wa chini, vinyozi, vikongwe, malaya, vichaa na wengine wa hali za chini.Wahusika wa namna hii kamwe wasingeweza kuonekana katika kazi mbalimbali za wanaurasmi. Msingi huu umejidhihirisha vyema katika kazi za fasihi mbalimbali kwa mfano, Tamthiliya ya NGUZO MAMA mwandishi katumia wahusika kama vile, Chizi ambaye ni muhusika wa hali ya chini anavyo shangaa Bi saba, kwani licha ya kuwa kiongozi hajui hata maana ya Nguzo mama. Vile vile katika riwaya ya USIKU UTAKAPOKWISHA.
MAFANIKIO YA ULIMBWENDE WA WASWAHILI
Japo ulimbwende wa waswahili haukuelezewa kinadharia ulikuwa tu katika kazi tofauti tofauti za waandishi wa kazi za fasihi wakiwemo Shaaban Robert, Shafi Adam Shafi pamoja na Mulokozi huku wakifanikiwa na mambo yafuatayo. Kuleta usawa katika maisha, kuwatumia wahusika wa ajabu, kutoa dhamira zinazozungumzia utu, mapenzi na haki za binadamu, na kutumia lugha ya kawaida.
UDHAIFU WA ULIMBWENDE WA WASWAHILI
Ulimbwende wa waswahili ingawa ulikuwa na mafanikio katika kazi zao pia ulikuwa na udhaifu kama ifuatavyo. Kazi zao nyingi zimejikita katika mapenzi pamoja na kukosa uhalisia wa kazi za kifasihi mfano, katika riwaya ya KUFIKIRIKA.
Baada ya kuangalia dhana hizi mbili kwa pamoja katika vipengele mbalimbali sasa ni vyema tukaangalia kiini cha swali letu, ambalo ni kulinganisha pamoja na kulinganua dhana hizi.
11
KUFANANA KWA ULIMBWENDE WA MAGHARIBI NA ULIMBWENDE WA WASWAHILI
Mfanano katika utoaji wa dhamira kwa jamii lengwa
Dhana hizi mbili yaani ulimbwende wa kimagharibi na ulimbwende wa waswahili wote walijikita katika kuelezea dhamira ambazo zinahusiana na mapenzi, utu, na uadilifu katika matendo ya wanadamu. Hivyo kazi nyingi za ulimbwende zilitungwa kwa kujikita katika kutetea maswala ya msingi ambayo yalijitokeza katika jamii. Mfano katika tamthiliya ya NGOSWE PENZI KITOVU CHA UZEMBE na diwani ya MAPENZI BORA ya Shaaban Robert.
Zote zinatumia lugha katika kazi za fasihi.
Walimbwende wa kimagharibi na walimbwende wa waswahili wote walitumia lugha katika kuwasilisha mawazo yao kwenye fasihi andishi ambayo lugha hiyo ilikuwa inatumia misemo, methali pamoja na nahau mbalimbali. Pia ilikuwa nyepesi ili kumrahisishia msomaji katika kutambua maudhui ya kazi hizo. Mfano kutokana na kazi mbalimbali za waasisi wa kimagharibi na waswahili kama vile Shaaban Robert, Penina Muhando, Wordworth William, pamoja na Coleridge Samuel.
Zote zinatumia wahusika wa ajabu.
Walimbwende wa kimagharibi na walimbwende wa waswahili, waasisi wote wanajikita katika utumizi wa wahusika wa ajabu kama vile, mazimwi, mashetani, machizi, na masokwe. Mfano mzuri unajitokeza karika riwaya ya CHOZI LASAMIRA iliyoandikwa na Farida Mvungi, pamoja na MADONDA NDUGU kilichoandikwa na Ally Alijai.
Pia ufanano unajitokeza katika utetezi wa haki za binadamu.
12
Hapa tunaona kuwa dhana hizi mbili zilijikita katika utetezi wa haki za binadamu ambazo zimejidhihirisha kupitia kazi mbalimbali za fasihi. Mfano, katika ulimbwende wa kimagharibi ambao uliibuka katika karne ya 18 mpaka 19 ambapo kulikuwa na unyanyasaji wa haki za binadamu kutokana na mapinduzi ya viwanda ya kipindi hiko. Pia katika kazi za waswahili ulimbwende uliibuka mnamo mwaka 1960 na kuendelea, kazi nyingi ziliandikwa kwa kupinga unyanya wa wakoloni.
Baada ya kuona mfanano wa dhana hizi mbili za ulimbwende ni vyema pia tukaangalia utofauti uliopo katika ulimbwende wa kimagharibi na wa waswahili.
UTOFAUTI WA ULIMBWENDE WA KIMAGHARIBI NA WA WASWAHILI
Utofauti katika tanzu za fasihi andishi.
Hapa dhana ya ulimbwende wa kimagharibi na wa waswahili unatofautiana katika tanzu za fasihi andishi. Mfano ulimbwende wa kimagharibi umejikita sana katika tanzu ya ushairi ambayo dhima yake kuu ni kusisimua na kuibua hisia za moyoni za wasomaji au anayekariri shairi. Ingawa ulimbwende wa waswahili umejikita hasa katika tanzu zote za fasihi andishi yaani, riwaya, tamthiliya pamoja na ushairi. Hivyo tanzu hizi zililenga kuibua mawazo ya kimapinduzi ya kisanaa ambayo yalilenga kuzikana sheria za wana urasmi mkongwe na ulimbwende mpya ambapo msanii hakuwa na uhuru katika kazi yake.
Utofauti katika waasisi wake
Dhana ya ulimbwende inajadiliwa na wataalamu tofauti tofauti ambao wametofautiana kimaeneo. Mfano ulimbwende wa kimagharibi waasisi wake ni Wordworth William na
13
Coleridge Samuel ambao walikuwa wakileta ukinzani dhidi ya urasmi mpya wa
kimagharibi na hasa baada ya mapinduzi ya viwanda. Hivyo kazi zao zililenga kutetea demokrasia na uhuru wa mtu dhidi ya utumwa, dhuluma za wanajamii wengi kupitia maswala waliotunga. Ingawa waasisi wa ulimbwende wa waswahili walikuwa ni Mulokozi, Shaaban Robert, Shafi Adam Shafi, Mohamed S. Khatib, pamoja na Penina Muhando ambao wanaibua mawazo ya kimapinduzi ya kisanaa ambayo yalilenga kuzikana sheria za urasmi mkongwe. Hivyo basi nadharia ya ulimbwende inaweza kujibainisha kwa misingi mbalimbali kupitia kazi zao za fasihi .
Utofauti katika kipindi cha utokeaji.
Ulimbwende wa kimagharibi umejitokeza katika vipindi viwili ambapo kipindi cha kwanza kilijitokeza karne ya 12 mpaka karne ya 13 ambapo kipindi hiki ulimbwende ulijikita katika fasihi simlizi. Pia kipindi cha pili kilijitokeza karne ya 18 mpaka 19 na hii ilitokana na mapinduzi ya viwanda huko magharibi. Ingawa ulimbwende wa waswahili ulijitokeza katika miaka ya 1960 na kuendelea mpaka sasa. Hivyo kazi nyingi zilijikita kupinga nyanja zote zilizokandamiza utu na haki za binadamu hasa katika tabaka la chini. Mfano wa kazi hizo ni riwaya VUTA NI KUVUTE ya Shafi Adam Shafi.
Utofauti katika uelezaji wa dhana ya ulimbwende.
Ulimbwende wa kimagharibi umeelezewa kinadharia zaidi na waasisi wake ambayo nadharia hiyo inajulikana kama nadharia ya ulimbwende wa kimagharibi. Ingawa katika ulimbwende wa waswahili hakuna nadharia inayodhihirisha ulimbwende huo wa waswahili, ila ulimbwende huu wa waswahili umejitokeza au kujidhihirisha katika kazi mbalimbali za fasihi andishi. Mfano tamthiliya ya KIVULI KINAISHI iliyoandikwa na
14
Mohamed S. Khatib pia CHOZI LA SAMIRA iliyoandikwa na Farida Mvungi.
HITIMISHO
Licha ya kuona utofauti na ufanano wa ulimbwende wa kimagharibi na ule wa waswahili, dhana ya ulimbwende imefanikiwa kuonesha sanaa yake katika nyanja zote yaani kiuchumi, kisiasa, kijamii pamoja na kiutamaduni. Ingawa kuna baadhi ya mapungufu yaliyo jitokeza katika dhana ya ulimbwende wakimagharibi na wa waswahili kama vile kuibuaka kwa migogoro kati ya wanamapokeo na wanamamboleo katika utanzu wa ushairi










15
MAREJELEO
Robart,S.(1991), Maisha Yangu na Baada ya Miaka Hamsini.Mkuki na Nyota Publishers: Dar es
Salaam.
Mayega,P.B.(2006). Mwalimu Mkuu wa Watu. MPB Enterprises: Dar es Salaam.
Ntarangwi,M.(2004) Uhakiki wa kazi za fasihi. Augustina College: Rock Island.


Copyright © 2024 DOKUMEN.SITE Inc.